Weekly Wisdom

Change the Life of The Youth to change the World.
Changes is not a miracle, its a preparation and commitment under high discipline.
Believing in Christ is the basic of Discipline.

Monday, January 27, 2014

Maana ya Pasaka na Maombi yake


Maana ya Pasaka na Maombi yake.
Mpendwa watu wengi sasa wanatamka pasaka lakini ajabu ni kwamba wanaitamka kwa desturi tu, wengine hata ukiwahoji pasaka maana yake nini hawaelewi chochote. Hakika laiti wangelijua maana ya pasaka wangeliomba mambo makubwa kabisa kwani ndo majira ambayo mageuzi makubwa yanafanyika kwa mwanadamu.
Maana ya Pasaka
Pasaka haikuanza baada ya kuzaliwa Kristo au baada ya mateso ya Kristo bali wakati wana wa Israeli wa lipokuwa Misri.
Kutoka 12:11 ...nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana.
Bwana alipokuwa anataka kuangamiza wazaliwa wa kwanza wa wana na wanyama wa wamisri akatafuta namna ya kuwaokoa wana wa Israeli kutoka maangamizi hayo na ndipo anawaamuru wachinje mnyama asiye na ila, damu yake wapake katika milango na wamle pasaka. Na wakakumbushwa wafanye hivyo kama ukumbusho vizazi na vizazi.
Kwanini Mateso ya Bwana Yesu Krito wa Nazareth yaitwe Pasaka?
Kwanza mateso yalitukia majira ya Pasaka ile sikukuu ya mikate isiyotiwa Chachu (Pasaka ya ukumbusho wa Bwana alivyowakoa kule Misri zidi ya maangamizi ya mzaliwa wa kwanza) Luka 22 :1-2 ikakaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo sikukuu ya pasaka. Na wakuu wa makuhani  na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua, maana walikuwa wakiwaogopa watu.
Kwa hiyo Mafarisayo walipanga kumuua majira ya pasaka japo waliogopa kuiharibu pasaka kwa sababu kuu moja kwamba kama wangemuua majira mengine nje ya pasaka basi wangesababisha kuwepo pasaka mbili yaani ile ya mikate isiyotiwa chachu na ya mateso na kuuawa kwa Bwana Yesu. Nasema hivi kwa sababu Pasaka ya kwanza ilikuwa taswira ya pasaka ya pili pasaka halisi ya ukombozi wa wanadamu wote.
Je kuna uhusiano wa Pasaka hizi mbili?
Ndio kwa sababu pasaka ya kwanza ilihitajika ili kuwaokoa wana wa Israel na pasaka ya mateso ya Kristo kwa ajili ya kuwaokoa wanadamu wote.
Mathayo 1:21 Naye atazaa mwana nawe utamwita jina lake Yesu,  yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
 Pasaka ya kwanza ilimhitaji mwanakondoo asiye na ila yaaani asiye na kosa wala jeraha na ya pili inamhitaji mtu asiye na ila, uovu wala jeraha katika maisha yake ndio Yesu Kristo wa Nazareti. Kwamba hakuwa na uovu haikuthibitishwa na wanafunzi wake( maana wangemtetea) bali alithibitisha Pilato mwenyewe.
Mathayo 27:24 …mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki… pia Luka 23: 22 … huyu ametenda uovu gani?....
Kwa hiyo Pasaka ni sikukuu ya ukombozi wa wanadamu si kuwaokoa tu kutoka dhambi bali kuwakomboa kutoka maangamizi ya Yule muovu Ibilisi pamoja na mateso yake maana Bwana Yesu aliteswa ili wanadamu wasiteseke akawa mtu wa huzuni wanadamu wawe na furaha na amani tele. Isaya 53 inafafanua vizuri kabisa mateso aliyopata Bwana yesu kwa ajili ya mwanadamu.
Maombi wakati wa Pasaka
Yamfaa mtu aombe kuokoka yaani amkiri Bwana Yesu Kristo wa Nazareti kuwa Bwana na mwokozi wa Maisha yake. Amtwike mizigo yake.
Mathayo 11:28. Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
 Baada ya kuokoka na kwa mwamini WAKATI WA PASAKA NDO MAJIRA MUHIMU SANA KWA MKRISTO NA YAMPASA  AOMBE MAMBO MUHIMU ZAIDI NA SI TU YALE ANAYOAMINI BWANA ATATENDA BALI YALE ANAYOHITAJI. Aombe mambo ambayo hayakuwezekana kwa miaka mingi lakini sasa autazame msalaba mahali ambapo Bwana Yesu alitamka alikamilisha wokovu.  Naandika hivi kwa kumaanisha kwa sababu kuna waamini wanaomba lile waloamimini Bwana anaweza kutenda kwa hiyo kama imani yake ni ndogo basi ataomba vitu vidogo vidogo tu, lakini aombe mambo anayohitaji yatokee, na Bwana atayafanya kwani aliwekwa msalabani kwa ajili ya mwanadamu siteseke tena.
Wako katika safari,
Mwl Peter Kapagi

Saturday, January 25, 2014

KIKAO CHA WARATIBU NA WALEZI TAYOMI MBEYA CHAFANA

Leo Jumamosi kumefanyika kikao cha waratibu na walezi TAYOMI-CASFETA NA BCF, kikao kimefanyika katika chumba cha mikutano kanisa la PHM kadege kuanzia saa 3:00asubuhi hadi Saa 9:00 alasiri.
Kikao hicho kimefana sana kikiongozwa na mratibu wa Mkoa C.G Kasalile na katibu Ask. Kazio pamoja na waratibu wengine Mwl.Nsojo, Mama mratibu wa BCF, Mhandisi Angumbwike na RTS Mgogo. Wajumbe walikuwa waratibu wa ngazi zote pamoja na walezi wa matawi mbalimbali ya CASFETA na BCF wakiwemo waratibu wapya ambao wamehitimu CASFETA akiwemo Mwl Veronica, Mwl Patrick, Dada Vaileth na wengineo wakiwemo walezi wasio na mipaka na vinguke wa CASFETA mkoa wa Mbeya Ndg Kapagi Mwl Mkongwe wa kwaya Dada Salome.
Kikao kilikuwa cha aina yake kwa kukutanisha mazao ya CASFETA watumishi ambao hawajaonana muda mrefu.
Ajenda mbalimbali zimejadiliwa zikitiwa chachu na ya Kambi la Pasaka, Umiliki wa uwanja pamoja na mikakati ya kuundeleza pamoja na ile ya account ya mkoa.
Maazimio muhimu ni pamoja na kuyafikia matawi mbalimbali kukagua uhai wa matawi hayo ikiwemo kuhamasisha mahudhuria ya kambi la Pasaka.
Mkoa wa Mbeya umejiandaa kufanya makambi matatu ya Pasaka katika vituo vya Jiji la Mbeya, Rungwe na Mbalali.
Bwana anatufanikisha sana kazi yako ni kupiga magoti na kuipeleka mikakati hii mbele ya Mungu kwa maombi.

Karibu TAYOMI na CASFETA

Bwana asifiwe.
Mpendwa na mdau wa TAYOMI na mikakati yake CASFETA, EEMC, BDF n.k ninayo furaha kukukaribisha katika blogu yetu. Hakika itakuwa blogu muhimu kwa habari na taarifa mbalimbali za TAYOMI.
Ubarikiwe
Mratibu Mbeya